Soma Biblia Kila Siku 10/2024Mfano
Uzia mwana wa Amazia alianza kutawala Yuda akiwa mdogo:Alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala; akatawala miaka hamsini na miwili huko Yerusalemu(m.2). Alifanya mengi yanayompendeza BWANA kama baba yake. Ila aliruhusu mwendelezo wa ibada iliyohusisha kutoa dhabihu kwa miungu.Mahali pa juu hapakuondolewa, nao watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu(m.4). Katika 2 Nya 26:16 na 19 imeelezwa jinsi Mungu alivyompiga Mfalme Uzia ukoma, huyu alipomwasi Mungu: [Uzia]alipokuwa na nguvu, moyo wake ulitukuka, hata akafanya maovu, akamwasi Bwana, Mungu wake; kwani aliingia hekaluni mwa Bwana, ili afukize uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia....Naye hapo alipowaghadhibikia makuhani [waliotafuta kumzuia asifukize uvumba], ukamtokea ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani nyumbani mwa Bwana. Tangu hapo alilazimika kukaa peke yake, mtoto wake Yothamu akitawala kwa niaba yake. Hili ni angalizo kwamba Munguhuwapinga wenye kiburi(1 Pet 5:5) na kuweza kuwashusha. Tutumie fursa, Mungu anapotupa nafasi ya kutubu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz