Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 10/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

SIKU 30 YA 31

Akiwa na miaka 20 Ahazi alianza kutawala Yuda. Alifanya machukizo mengi mbele ya Mungu.Akatawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu; wala hakufanya mema machoni pa Bwana Mungu wake, kama Daudi babaye. Lakini aliiendea njia ya wafalme wa Israeli, hata akampitisha mwanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli. Kisha akatoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti mbichi.... Ahazi akatuma wajumbe kwa Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akasema, Mimi ni mtumishi, tena mwana wako; kwea, ukaniokoe mkononi mwa mfalme wa Shamu, na mkononi mwa mfalme wa Israeli, walioniinukia(m.2-4, 7). Pamoja na kutoa sadaka na uvumba kwa miungu, alimtoa mtoto wake kafara, na akatafuta msaada kwa mfalme wa Ashuru wakati wa vita badala ya kumkimbilia Mungu. Tunaona hawa wafalme wa Israeli na Yuda waliitegemea misaada ya wafalme wageni badala ya kumtafuta Mungu. Tusiwaige. Tupatapo shida tusiwategemee wanadamu. Tumtafute BWANA wa mbingu na nchi, ndipo tutabarikiwa:Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda(Yer 17:7-8).

siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz