Soma Biblia Kila Siku 10/2024Mfano
Peka alitawala miaka 20 katika Israeli. Huyu naye alifanya mengi ya kumchukiza Mungu na hivyo aliwakosesha Waisraeli. Mfalme wa Ashuru alimshukia na kuteka maeneo mengi, na waliokaa hapo akawapeleka uhamishoni. Hoshea alifanya fitina akamwua Peka, akatwaa utawala. Katika Yuda, Mfalme Yothamu alianza kutawala Mfalme Peka akiwa na miaka 2 ya utawala. Alifanya mema mbele za Mungu, japo naye hakuondoa ibada za miungu kama walivyofanya watangulizi wake. Tujihadhari na kurudia dhambi za baba zetu:Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao(Omb 5:7).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz