Soma Biblia Kila Siku 10/2024Mfano
Mfalme Amazia wa Yuda alianza utawala wake vizuri.Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, ila si kama babaye Daudi; akafanya kama yote aliyoyafanya baba yake Yoashi(m.3). Angalia habari hiyo kuhusu kutokutenda kama alivyofanya Daudi, baba yao. Tofauti kubwa ni kuruhusu ibada za kutoa dhabihu kwa miungu kuendelea kwenye milima nchini, kama ilivyoelezwa katika m.4:Mahali pa juu hapakuondolewa; watu wakaendelea kutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu. Hii inaonesha kuwa ni vema kutenda mema kwa kufuata misingi ya watangulizi wetu waliomtegemea Mungu. Hivyo tutadumu mahali anapoudhihirishawingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu(Efe 2:7).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz