Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano
Yehoashi akimwita nabii Elisha “Gari la Israeli na wapanda farasi wake”, huenda anafikiri juu ya hali mbaya ya jeshi la Israeli. Kumbuka ilivyoandikwa katika m.7: [Mfalme wa Shamu]hakumwachia Yehoahazi watu ila wapandao farasi hamsini, na magari kumi, na askari elfu kumi waendao kwa miguu; kwa kuwa mfalme wa Shamu aliwaharibu, akawaponda mfano wa mavumbi yaliyokanyagwa.Huenda Mfalme Yehoashi alielewa kuwa mlinzi wa kweli wa nchi ni Bwana wa majeshi. Tendo la kupiga mshale linamaanisha utabiri wa ushindi wa Waisraeli. Nabii Elisha alikufa wakati wa utawala wa Yehoashi, lakini matukio ya ajabu katika kaburi lake yalionesha kuwa Mungu aliyefanya kazi kupitia Elisha, bado yu hai na mwenye nguvu. Huthibitishwa pia na kutimia kwa utabiri wa ushindi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz