Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

SIKU 24 YA 30

Walinzi walimlinda Yoashi wakati Yehoyada aliongoza ibada ya kumsimika. Athalia alipoona akalia,Fitina, lakini hawakuonekana watu waliomwunga mkono. Badala yake tunasoma katika m.17-18 kwambaYehoyada akafanya mapatano kati ya Bwana na mfalme na watu, ili wawe watu wa Bwana; tena kati ya mfalme na watu. Watu wote wa nchi wakaiendea nyumba ya Baali, wakaiangusha; madhabahu zake na sanamu zake wakazivunja-vunja kabisa. Habari hizi zote zinaonyesha kuwa jambo kubwa halikuwa kumtawaza Yoashi, bali kuhakikisha Wayudi waendelee kuwa watu wa Bwana, na dini ya Ubaali aliyoleta Athalia isiwepo. Furaha ya watu inaonyesha kuwa ndivyo walivyotaka kwa moyo. Furaha ni tunda la Roho (Gal 5:22:Tunda la Roho ni upendo, furaha ...). Je, unafurahi katika Bwana anaposimikwa mtumishi wa Mungu?

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana