Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Mfalme Yosia alijaribu kuwazuia Wamisri wasiwasaidie Waashuri, kwa kuwa aliuhofia muungano wao kuwa ungekuwa hatari kwa Yuda. Wayuda wakaingia vitani bila kumwuliza Mungu wala kupata kibali chake. Jambo hilo lilimwudhi Mungu, hivyo akaamua kuadhibu.Bwana akasema, Nitawahamisha Yuda pia mbali nami, kama nilivyowahamisha Israeli, nami nitautupa mji huu niliouchagua, naam, Yerusalemu, na nyumba ile niliyoinena, Jina langu litakuwa humo(m.27). Kama matokeo yake, Yosia aliuawa vitani mwaka 609 K.K., na wanawe wakabadilishana utawala. Uongozi bila Mungu siku zote na mahali popote huwa ni changamoto, tena matokeo yake yangeweza kudumu muda mrefu, kama ilivyodokezwa katika m.26:Bwana hakuuacha ukali wa ghadhabu yake nyingi, ambayo kwayo hasira yake iliwaka juu ya Yuda, kwa sababu ya machukizo yote ambayo Manase amemchukiza.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz