Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Mfalme Yekonia anarudia kosa la kuacha kuitetea Yerusalemu kwa kumtegemea Mungu, naye anaamua kujisalimisha kwa mfalme wa Babeli badala ya kumwuliza Mungu kwanza. Ndipo ufalme na mali zote zinapelekwa utumwani Babeli. Mkristo akiishi maisha yake nje ya Kristo ni mlango wazi kwa kuchukuliwa na kutumikishwa na shetani. Mungu ametufunulia kwamba kiroho mwisho wa maisha hayo ni mabaya, hata kama kwa mtazamo wa kibinadamu yangeonekana kustawi kifikra na kiuchumi hadi mtu afariki dunia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz