Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Ni mara ya pili Wababeli kuliteka mji wa Yerusalemu. Uovu wa Yuda ulisababisha vifaa vya hekalu kuharibiwa na sehemu zake zenye thamani kuchukuliwa mateka. Viongozi nao wakachukuliwa mateka. Ni kawaida kwamba viongozi wa kanisa wanapofanya yasiyofaa, wanasababisha ibada zisiwe na nguvu ya Mungu, na hivyo waumini huanza kufanya wanavyojisikia. Mkristo, kumbuka kuwaombea viongozi wako wa kanisa na hata wa nchi, ili wewe na jamii yako mbaki salama. Kinyume na hapo hamtakuwa salama.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz