Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Sheria haimhusu mtu wa haki(m.9), maana yake ni nini? Jibu ni kwamba tunaokolewa kwa neema. Haki yetu yapatikana kwa kumwamini Yesu Kristo. Si kwa matendo, kwa sababu hakuna awezaye kutimiza sheria. Kazi ya sheria ni kutuonyesha makosa yetu ili tutubu dhambi zetu na kumtegemea Kristo tu. Alifanya yale tuliyoshindwa kufanya alipokufa msalabani. Hii ndiyo habari njema inayokubaliwa na sheria, kwamba tuko huru toka mashtaka yake. Umkubali Yesu Kristo kama mwokozi wako, nawe utakuwa na amani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz