Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Wababeli na Wamisri walipigana ni nani awe na mamlaka juu ya Yuda. Katika hali hii Yeremia alikuwa miongoni mwa manabii waliokumbusha kumtegemea Mungu kuliko kuwategemea wanadamu (maneno haya katika m.2,neno la Bwana alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii,yanadokeza kwamba walikuwepo pia manabii wengine waliojulisha neno la hili). Mara kadhaa Yeremia alionya juu ya taifa la Mungu kuwategemea wanadamu. Kwa mfano anauliza katika Yer 2:18,Una nini utakayotenda katika njia iendayo Misri, kunywa maji ya Shihori? Au una nini utakayotenda katika njia iendayo Ashuru, kunywa maji ya ule Mto?Tena katika Yer 2:36 anauliza,Mbona unatanga-tanga hivi upate kugeuza mwendo wako? Utaona haya kwa ajili ya Misri pia, kama ulivyoona haya kwa ajili ya Ashuru. Ukristo ni ufuasi na uanafunzi wetu kwa Yesu Kristo. Ni jambo la kusikitisha sana pale mkristo anapokutwa na changamoto, kisha akaamua kumwacha Kristo na kujenga matumaini kwa wanadamu wasiokuwa na Mungu. Zingatia ilivyoandikwa katika Zab 118:9,Ni heri kumkimbilia Bwana. Kuliko kuwatumainia wakuu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz