Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Yosia aliamua kusafisha hekalu na kurekebisha ibada zote za Israeli zimwelekee Yahweh.Mfalme akamwamuru Hilkia, kuhani mkuu, ... kwamba watoe katika hekalu la Bwana vyombo vyote vilivyofanywa kwa ajili ya Baali, na kwa ajili ya Ashera, na kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni .... Akawaondosha wale makuhani walioabudu sanamu .... Naye akaiondoa Ashera katika nyumba ya Bwana, ....Akawaondoa farasi ambao wafalme wa Yuda waliwatoa kwa jua .... Nazo madhabahu zilizokuwako darini juu ya chumba cha juu cha Ahazi, wafalme wa Yuda walizozifanya, nazo madhabahu alizozifanya Manase katika behewa mbili za nyumba ya Bwana, mfalme akazivunja .... Akazivunja-vunja nguzo, akayakata-kata maashera, ...(m.4-6, 11-12, 14). Akawahamasisha watu wote kufanya upya maagano na Mungu:Mfalme akatuma wajumbe, nao wakamkusanyia wazee wote wa Yuda na wa Yerusalemu. ... akasoma masikioni mwao maneno yote ya kitabu cha agano kilichoonekana katika nyumba ya Bwana. ... akafanya agano mbele za Bwana, kumfuata Bwana, na kuyashika maagizo yake, na shuhuda zake, na amri zake, kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kuyathibitisha maneno ya agano hilo yaliyoandikwa katika kitabu hicho; nao watu wote wakalikubali agano lile(m.1-3). Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, lakini mara nyingi maisha yetu yamekuwa na michanganyo ambayo Mungu hafurahiwi nayo. Somo la leo litukumbushe kuchukua hatua ya kujisafisha kutupa nje yasiyompendeza Mungu na kuishi maisha yale mapya yanayotokana na kumwamini na kumfuata Kristo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz