Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano
Ili kulielewa vema somo hili yafaa kukumbuka vifungu vya Mdo 7:44 na Ebr 8:5 na 1-2:Ile hema ya ushahidi ilikuwa pamoja na baba zetu jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema na Musa, ya kwamba aifanye sawasawa na mfano ule aliouonakatika mlima. … Na waliotoa sadaka kipindi hichowalitumikia mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni. …Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. Utengenezaji wa mahali patakatifu ulilenga pawe picha ya kuonyesha ukamilifu wa uhusiano endelevu kati ya Mungu na watu wake. Sasa Agano Jipya linasema kwamba Mungu hapatikani hemani:Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono(Mdo 17:24). Bali mwili wa Yesu ni hekalu lake, kama Yesu anavyoeleza katika Yn 2:19-21,Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha.Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake. Yesu Kristo ndiye Imanueli, yaani Mungu aishiye na watu wake. Yesu Kristo ameondoa lile pazia la hema ya kukutania lililokuwa linazuia watu wasikutane na Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/