Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2024

SIKU 26 YA 29

Mungu mtakatifu anawaita watu wake washiriki katika huduma yake takatifu. Katika huduma hii mavazi yalikuwa na maana kubwa. Kwanza, Mungu alimtambulisha Kuhani Haruni kwa njia ya mavazi yake, ili huyu asife alipomkaribia Mungu na kufanya huduma.Nayo itakuwa juu ya Haruni akitumika; na sauti ya hizo njuga itasikilikana hapo aingiapo ndani ya mahali patakatifu mbele ya Bwana na hapo atokapo nje, ili kwamba asife....Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake(m.35 na 43). Pili, kwa jinsi ya kimfano, kile kibati cha dhahabu alichovaa Haruni kwenye paji la uso wake kitachukua lawama ya makosa yanayofungamana na vitu ambavyo watu walimtolea Mungu.Litakuwa katika kipaji cha uso cha Haruni, na Haruni atauchukua uovu wa vile vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu, nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso sikuzote, ili kwamba vipate kukubaliwa mbele za Bwana(m.38). Siku hizi si suala la mavazi fulani, bali kumvaa Kristo.

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2024

Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/