Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano
Mavazi ya kikuhani yaliwakilisha hali ya utakatifu wa Mungu na kutakiwa kuakisi utukufu na uzuri wake (m.40,Utafanya kanzu kwa ajili ya wana wa Haruni, nawe wafanyie mishipi, wafanyie na kofia kwa utukufu na uzuri). Siku hizi Yesu Kristo ndiye kuhani mkuu, na Wakristo wote wanaomfuata ni makuhani waliowekwa wakfu kwa ubatizo na imani ili watangaze mambo makuu ya Mungu, kama ilivyoandikwa katika 1 Pet 2:9,Ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu. Hakuna sheria kuhusu kuvaa mavazi maalumu, ila katika maisha na huduma yetu yote tuonyeshe kwamba tumemvaa Kristo. Ushuhuda wetu unapata maana na nguvu pale tunapothubutu kuiendea neema ya Kristo Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/