Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano
Waisraeli walipoingia katika ua lililozunguka hema la ibada walikutana kwanza na madhabahu ya sadaka za kuteketezwa (kafara). Utaratibu wa kutoa sadaka hizi ulikuwa wa daima. Kuwepo kwa kafara ya kila mara kuliwakumbusha watu kwamba haiwezekani kumfikia Mungu pasipo kumwaga damu. Lakini kutoa kafara hakuwezi kuondoa dhambi na kuzifuta:Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi?Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka.Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi(Ebr 10:1-4). Yesu tu ndiye kafara kamilifu, ya kweli na ya kudumu milele. Yesu yupo, na kuwepo kwake ni mwisho wa wanadamu kutoa kafara. Hali iliyopo sasa ni kama ilivyoelezwa katika Ebr 10:12-14:Huyu [Yesu], alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake.Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/