Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano
Mungu anawapa watu wake mwongozo wa kuiteka nchi ya ahadi. Safari hii ina ulinzi wa Mungu ulio madhubuti sana (ling. Isa 52:11-12,Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana.Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia, kwa sababu Bwana atawatangulia; na Mungu wa Israeli atawafuata nyuma; awalinde). Mungu anapenda kuyaongoza maisha yako yote. Safari ya maisha ina changamoto mbalimbali zinazoambatana na majaribu na hofu ya kukosa usalama. Kuna usemi usemao “Msafiri kafiri”. Ni furaha yetu kuwa Mungu ametuahidi kutupatia ulinzi na usalama dhidi ya adha za safari. Yeye akiwa Alfa na Omega wa maisha yako,atakulinda ... tangu sasa na hata milele(Zab 121:8).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/