Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano
Uhusiano kati ya Mungu na watu wake unagusa hali nzima ya maisha. Mungu anatakakukaa kati yao(m.8). Hivyo panahitajika mahali pa Mungu kukutania nao, na Waisraeli wamtolee Mungu vitu vyote vitakavyotumika kwa kumjengea nyumba. Lakini angalia ilivyoandikwa!Kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu(m.2). Atoe kwa hiari yake na kwa kadiri alivyofanikiwa. Tukumbuke pia kuwa matoleo haya yalitoka kwa Mungu:Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi.Bwana akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara(Kut 12:35-36). Jihoji ukizingatia 1 Nya 29:17 na 2 Kor 9:7-8:Najua, Mungu wangu, ya kuwa wewe wajaribu moyo, nawe wapendezwa na unyofu. Nami katika unyofu wa moyo wangu nimeyatoa haya yote kwa hiari yangu mwenyewe; nami sasa nimeona kwa furaha watu wako, waliopo hapa, wakikutolea kwa hiari yao. …Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/