Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano
Ujenzi wa mahali patakatifu una mahitaji na kanuni zake maalumu. Yote yameamriwa na Mungu. Sanduku la Agano ni kitu cha msingi kinachopaswa kuwamo katika nyumba ya ibada, maana mahali hapo ndipo pa kukutana na Mungu, kama alivyosema mwenyewe,Nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda(m.22). “Kiti cha rehema” ni mahali pa upatanisho. Hufunika ule ”ushuhuda” (amri za Mungu). Kwa hiyo ni mahali pa kupokelea ukombozi na hata baraka. Lakini sasa, Mungu hakai katika majengo. Je, tunaweza kukutana naye wapi, na anataka kukaa wapi?Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli(Yn 1:14; tafsiri ya moja kwa moja ya neno la asili kwa “akakaa” ni “akapiga hema”).Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?(1 Kor 3:16).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/