Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano
Yesu alikwisha waambia wanafunzi wake kwamba baada ya kuuawa atafufuka siku ya tatu.Kwa mfano katika Mt 16:21 imeandikwa,Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Lakini kati ya maneno yote ya Yesu, neno hilo ndilo lilikuwa gumu zaidi kwao kuamini!Kwa maana walikuwa hawajalifahamu bado andiko, ya kwamba imempasa kufufuka(m.9). Lakini baadaye wakaelewa na kuhubiri kwamba hata tukio hilo limetabiriwa na manabii -ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko(1 Kor 15:4)! Kama neno la ufufuo lilionekana ni kweli, je, tuna sababu yoyote kuwa na mashaka juu ya maneno yake mengine?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Yohana na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/