Mwongozo wa KiMunguMfano
Amini
Ninaishi Oklahoma ambapo hali ya hewa inaweza kubadilika wakati wowote na haraka sana. Mwaka mmoja mwezi Machi, tulikuwa na siku yenye jua zuri sana wakati wa kiangazi na joto kufikia nyuzi joto 83. Siku hiyo hiyo kukatokea theluji yenye ukubwa wa inchi tatu. Kama mabadiliko ya ghafla yalivyokuwa, hakuna cha kulinganisha na wakati wa kimbunga. Kimbunga huwa kinazuka tuu pasipo kujua kinatokea wapi.
Kama zinavyofanya katika maisha yetu.
Nilizungumza na mwanamke mmoja kwenye mchezo wa mpira wa mwanangu hivi karibuni ambaye amekuwa akipambana na afya yake siku za karibuni. Alieleza jinsi alivyokuwa karibu na Mungu miaka iliyopita na alivyokuwa anatumika kanisani kwetu. Lakini alipoanza kupitia majaribu, alijiuliza Mungu anawezaje kuruhusu hili. Akazuia machozi yasitoke na kusema, " Nawezaje kumwabudu Mungu ambaye siwezi kumwamini?"
Tutamuamini Mungu ni mwema hata kama maisha mabaya?
Swali la mwanamke huyu linagonga katika moyo wa maamuzi makubwa ya maisha. Tuamini Mungu ni mwema hata kama maisha mabaya? Mwitikio wetu kwenye maumivu na changamoto huamua sana kuhusu mustakabali wetu.
Kwa asili yake, imani inahitaji uaminifu katika jambo fulani--au mtu fulani--ambayo haieleweki wala kutabirika katika viwango vya kibinadamu. Kama tu wakweli, wengi wetu tunataka ushahidi usiopingika wa uwepo wa wema wa Mungu katika maisha yetu.
Hii si mpya. Kumbuka Tomaso. Baada ya Yesu kufa msalabani na kufufuka tena kutoka kwa wafu, Tomaso alisema hataamini mpaka atakapoona uthibitisho. Badala ya kumkasirikia na kumtenga kwa kukosa kwake imani, Yesu kwa upole alimuonesha mikono iliyopigiliwa misumari.
Na kumbuka wanafunzi katika dhoruba?Basi, dhoruba kali ikaanza kuvuma, mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikaanza kujaa maji. Marko 4:37. Katikati ya dhoruba wanafunzi hawakuwa peke yao. Marko anatukumbusha katika mstari unaofuatia kwamba Yesu alikuwa sehemu ya nyuma ya mashua amelala.
Ukiwa na Yesu kwenye mashua yako, dhoruba bado zitakupiga, lakini hutazama.
Watu kama wewe na mimi, mwanamke katika mchezo wa mpira, Tomaso, na wanafunzi hufikiria kwamba hatuwezi kupitia dhoruba kama kweli Mungu yuko nasi. Lakini sivyo. Ukiwa na Yesu chomboni, bado dhoruba itakupiga, lakini hutazama. Yuko pamoja na wewe, wakati wa mvua na katika kimbunga kibaya.
Siyo tuu yuko na wewe, yupo kwa ajili yako. Na kama yuko kwa ajili yako, nani anaweza kuwa kinyume nawe? Mtumaini Mungu kwa chochote ulichokuwa umekishikilia. Mtumaini kwa mwenzi wako ajaye. Mtumaini kwa watoto wako, mtumaini kwa afya yako, mtumaini kwa kazi yako. Mtumaini kwa fedha zako.
Tumaini pasipo shaka.
Basi.
Omba: Baba wa mbinguni, nakutumaini kwa nitakachoanza nacho na kumaliza nacho. Ninakutumaini kwa nitakapokaa na kuondoka. Ninakutumaini vya kutosha kunipa uhai kutumika na kuungana na watu. Na nakutumaini upo kwa kusudi katikati ya dhoruba za maisha yangu. Asante kwa kuwa pamoja na mimi, kuongoza hatua zangu, na kunipa muelekeo wa kiungu. Amen.
Kuhusu Mpango huu
Kila siku tunafanya maamuzi ambayo yana unda hadithi ya maisha yetu. Maisha yako yangekuwaje kama ungekuwa bingwa wa kufanya maamuzi? Kwenye Mpango wa Biblia wa Mwongozo wa kimungu, mwandishi mzuri wa New York Times na Mchungaji Kiongozi, Craig Groeschel, anakutia moyo na kanuni saba kutoka kwenye kitabu chake cha Mwongozo wa Kimungu ili kukusaidia kupata busara ya Mungu kwa maamuzi yako kila siku. Gundua mwongozo wa kiroho unaohitaji ili kuishi hadithi ya maisha ya kumheshimu Mungu utakayopenda kuhadithia.
More