Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwongozo wa KiMunguMfano

Divine Direction

SIKU 3 YA 7

Kaa

Nimefikiria mara nyingi kuhusu maisha yangu yangekuwa tofauti kama ningekata tamaa nilipotaka. Habari yangu ingekuwa kama, " Nilikuwa nadhani nilitakiwa kuwa mchungaji, lakini nilikata tamaa na mambo hayakuwa. Hivyo ndivyo inavyokuwa." Nina uhakika lazima ushindane na changamoto zinazotokea katika nyakati mbalimbali za maisha yako: Bosi ambaye unadhani kesho haitafika, mahusiano ambayo ghafla yanaumiza, ndoto ambayo inakosa rasilimali, hatua ambayo ilikuvunja matarajio yako. Unapokumbana na magumu, ni kawaida kufikiria ukubwa wa maamuzi yaliyobadilisha maisha yako. Unaweza ukajiuliza maswali kama haya.

  • Je, nichukue hii kazi, niache hii niliyonayo, na nitafute nyingine?
  • Baada ya mahusiano ya mke wangu--ni wakati wa kuendelea na maisha yangu?
  • Nimevunjika moyo kuendelea na biashara? Nipunguze hasara kabla mambo hayajawa mabaya zaidi?
nisimame au niende zangu?

Ninaamua kuacha kwa sababu ni uamuzi sahihi au kuondoka ndiyo itakuwa rahisi zaidi?

Mara nyingi njia bora na yenye tija unayoweza kuchagua ni kuendelea hata kama ni rahisi kugeuka na kuondoka. Sisemi hutaweza Kutaka kuondoka. Lakini kabla ya kuamua, jiulize, " Ninachagua kuacha kwa sababu ni njia nzuri au kwa sababu kuondoka itakuwa rahisi?" Wakati mwingine tendo kuu la imani ni uaminifu, kubaki ulipopandwa. Miaka mingi ijayo tokea sasa unaweza kutazama nyuma na kumshukuru Mungu kwamba uliamua kusimama mahali ambapo ilikuwa rahisi kuondoka.

Kumbuka, Mungu alikuumba kwa sura yake na yeye ni mwanzilishi na mkamilishaji wa hadithi yako. Wewe si mkata tamaa. Wewe ni mmalizaji.

Omba: Mungu, kuja jambo nataka kukimbia kutoka kwenye kile unachotaka nibaki na kukamilisha? Utanipa nguvu ya kuendelea? Amen.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Divine Direction

Kila siku tunafanya maamuzi ambayo yana unda hadithi ya maisha yetu. Maisha yako yangekuwaje kama ungekuwa bingwa wa kufanya maamuzi? Kwenye Mpango wa Biblia wa Mwongozo wa kimungu, mwandishi mzuri wa New York Times na Mchungaji Kiongozi, Craig Groeschel, anakutia moyo na kanuni saba kutoka kwenye kitabu chake cha Mwongozo wa Kimungu ili kukusaidia kupata busara ya Mungu kwa maamuzi yako kila siku. Gundua mwongozo wa kiroho unaohitaji ili kuishi hadithi ya maisha ya kumheshimu Mungu utakayopenda kuhadithia.

More

Kungependa kumshukuru mchungaji Craig Groeschel na LifeChurch.tv kwa kuweshesha mpango huu Kwa maelezo zaidi tafadhali temembelea: http://craiggroeschel.com/