Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwongozo wa KiMunguMfano

Divine Direction

SIKU 1 YA 7

Anza

Kila siku tunafanya maamuzi ambayo yana unda hadithi yetu ya maisha. Maisha yangekuwaje kama unge achia kanuni za Mungu ziongoze maamuzi yako? Kwa wiki ifuatayo, tutaanza kuchunguza kanuni kutoka kwenye kitabu changu cha Mwongozo wa ki Mungu kukusaidia kupata hekima ya Mungu kwa maamuzi yako kila siku.

Kama mtu akikuuliza umwambie hadithi ya maisha yako ungejibu nini?

Unaweza kuanza na ulipo zaliwa na jinsi ulivyo kuzwa. Unaweza kutaja mpenzi wako wa kwanza. Labda utaongelea kitu kikubwa familia yako ilichofanya au ulivyo acha chuo. Kama una ndoa utanza kueleza jinsi ulivyo kutana na mwenzi wako. Kama hauna ndoa utaelezea kwanini. Kama ni mzazi unaweza kuchukua simu yako kuonesha picha za familia yako. Au labda utaelezea kazi yako. Kuna nini kwenye hadithi yako?

Wengi wetu kuna sura ambazo tusingependa kushirikisha mtu yoyote. Labda umeishia sehemu ambayo hukutaka kuwepo. Hukumaanisha kuharibu ila uliharibu. Ulifanya maamuzi ambayo yalikupeleka mbali zaidi na unapotaka kwenda. Ulifanya kitu ambacho kiliku gharimu kuliko ulivyo fikiri utalipa. Umeumiza watu. Ulikubali kushusha thamani yako. Ulivunja ahadi. Ulifanya vitu ambavyo unahisi huwezi kuvifuta.

Hadithi yako haijaisha. Hujachelewa kubadilika ili kubadilisha hadithi utakayo elezea siku moja.

Kuna habari nzuri: Hadithi yako haijaisha.Hujachelewa kubadilika ili kubadilisha hadithi utakayo elezea siku moja. Haijalishi ulichokifanya (au hujafanya), siku zako zijazo bado hazija andikwa. Una ushindi mwingi wa kushinda, marafiki zaidi kukutana nao, utofauti wa kufanya, uzuri wa Mungu kuuona. Hata kama unapenda au haupendi kubadilika sasa, kwa msaada wa Mungu, unaweza kubadilisha hadithi iwe ambayo unajisikia fahari kuhadithia.

Njia moja ya kubadilisha hadithi yako: anzakitu kipya.

Haijalishi kama unajisikia hujiamini, kuogopa, kusimama sasahivi, hadithi yako inaendelea leo. Utaanza ninileo? Kusali kila siku na mwenzi wako? Kusoma Mpango wa biblia ya YouVersion kila siku? Kupata ushauri nasaha kutatua suala ambalo halijatatuliwa? Kuishi kwa ukarimu? Kuhudumu kanisani au kwenye jamii? Huu ni mda mzuri wa kuandika haraka. Fungua daftari andika mawazo yako. Usifikirie sana kuhusu hili. Lakini pata wakati uandike kwenye karatasi. Sentensi moja au mbili.

Jiulize: Nahitaji nini kuanza ili kwenda kwenye mwongozo wa hadithi ya maisha ninayotaka kuhadithia?

Jifunze zaidi kuhusu kitabu changu, Mwongozo wa ki Mungu.

Mpango huu wa Bibilia umechukuliwa kutoka kwenye kitabu cha, Mwongozo wa ki Mungu, na ruhusa kutoka Zondervan. Yaliyomo yamebadilishwa kwa umakini.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Divine Direction

Kila siku tunafanya maamuzi ambayo yana unda hadithi ya maisha yetu. Maisha yako yangekuwaje kama ungekuwa bingwa wa kufanya maamuzi? Kwenye Mpango wa Biblia wa Mwongozo wa kimungu, mwandishi mzuri wa New York Times na Mchungaji Kiongozi, Craig Groeschel, anakutia moyo na kanuni saba kutoka kwenye kitabu chake cha Mwongozo wa Kimungu ili kukusaidia kupata busara ya Mungu kwa maamuzi yako kila siku. Gundua mwongozo wa kiroho unaohitaji ili kuishi hadithi ya maisha ya kumheshimu Mungu utakayopenda kuhadithia.

More

Kungependa kumshukuru mchungaji Craig Groeschel na LifeChurch.tv kwa kuweshesha mpango huu Kwa maelezo zaidi tafadhali temembelea: http://craiggroeschel.com/