Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwongozo wa KiMunguMfano

Divine Direction

SIKU 2 YA 7

Simama

Moja ya maamuzi bora unayoweza kufanya unapokabiliana na jiapanda ya jambo fulani ni uamuzi wakusimama. Tulia kwa muda. Omba kwa ajili ya uongozi wa Mungu. Ulale nalo. Pata hekima ya Mungu kutoka kwa watu unaowaamini na ufikirie yanayoweza kutokea. Ndipo, jiulize, " je ni jambo la kusimama kabisa?"

Wengi wetu tuna lengo jema ama angalau uhalali fulani kwa mambo tunayoyafanya. Lakini bado wengi wetu tunaonekana kushangaa tunapojikuta tuko mbali sana na mwelekeo tuliotaka kwenda. Mabadiliko makubwa katika maisha yetu--yawe hasi ama chanya--hayatokei bila kuwa na msululu wa maamuzi yaliyopandana kama dhumna.

Unaona jinsi ambavyo kusimama kunaweza kuwa jambo la maana kufanya? Unaposimama na kujua ulipo na unapotaka kwenda,ndipo unaweza kuamua jinsi ya kuendelea kuelekea hatima yako..

Utaacha nini ili kufikia karibu na muelekeo wa kiungu?

Unafanya kitu kinachokupeleka katika uelekeo usioutaka kwenda ( au Mungu hataki uende)? Unahitaji nini ili uweze kusimama au kuacha moja kwa moja? Mazoea ya mitandao ya kijamii, pombe, picha za ngono, kibali ama kazi? Mahusiano yasiyokuwa na afya? Tabia ya kuhukumu? Utaacha nini ili uweze kusogea karibu na uelekeo wa kiungu? Chukua kila uamuzi kama hatua inayofuata kuelekea hatima yako.

Wakati tabia au mahusiano yanatupeleka mweleko ambao tunajua unatutoa mbali na hadithi tunayotaka kuieleza, tunahitaji kusimama siyo tuu kutafakari athari zake lakini pia kuacha kusafiri mwelekeo usio sahihi. Yawezekana umesikia neno "Tubu". Moja ya maana halisi ni kugeuka. Unapotubu, unaacha kuelekea upande mmoja na kumrudia Mungu na njia yake kwa ajili yako.

Katika sentensi hizi, kuacha maana yake kuelekea mwelekeo mpya. Unaweza kutaka kuelekea kwenye kuwajibika, msamaha, marafiki sahihi, au sehemu mpya ya kuishi.

Jiulize:

1. Nikifanya uchaguzi naoufikiria, utanipeleka wapi?

2. Niache nini ili niweze kuelekea karibu na mwelekeo wa kiungu?

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Divine Direction

Kila siku tunafanya maamuzi ambayo yana unda hadithi ya maisha yetu. Maisha yako yangekuwaje kama ungekuwa bingwa wa kufanya maamuzi? Kwenye Mpango wa Biblia wa Mwongozo wa kimungu, mwandishi mzuri wa New York Times na Mchungaji Kiongozi, Craig Groeschel, anakutia moyo na kanuni saba kutoka kwenye kitabu chake cha Mwongozo wa Kimungu ili kukusaidia kupata busara ya Mungu kwa maamuzi yako kila siku. Gundua mwongozo wa kiroho unaohitaji ili kuishi hadithi ya maisha ya kumheshimu Mungu utakayopenda kuhadithia.

More

Kungependa kumshukuru mchungaji Craig Groeschel na LifeChurch.tv kwa kuweshesha mpango huu Kwa maelezo zaidi tafadhali temembelea: http://craiggroeschel.com/