Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwongozo wa KiMunguMfano

Divine Direction

SIKU 6 YA 7

Unganisha

Nilipotambua kwamba niliumbwa siyo tuu kutumika kanisani, bali kuwatumikia na wengine kama kanisani, kuunganika na watu likawa ni jambo muhimu. Huwezi kutumika bila kuunganika. Na unayeunganika naye atabadilisha habari yako kesho. Hili limekuwa kweli katika historia yote. Hebu fikiria mtu aliyeandika theluthi moja ya Agano Jipya, mtume Paulo.

Paulo siku zote hakuwa mkristo. Kabla ya kuwa mfuasi wa Yesu, alikuwa Sauli kutoka katika mji ulioitwa Taso, mtu mwenye hasira aliyewatesa na kuwaua wakristo. Kama hupendi makundi ya Yesu, ungempenda Sauli. Lakini baada ya kupoteza maisha ya wale waliomuamini Yesu alifufuliwa kutoka kwa wafu, Paulo akawa mmoja wao.

Mabadiliko yake yalikuwa makubwa sana, ya ghafla, ya kubadilisha maisha kwamba Sauli ( aliyeitwa Paulo) ghafla akataka kuwaambia wengine habari za Yesu. Tatizo lilikuwa hakuna wakristo waliomuamini kwa sababu za wazi.

Kitabu cha Matendo kinaeleza kirahisi:wakati [Saul] alipokuja Yerusalemu, alijaribu kuungana wa wanafunzi, lakini wote walimwogopa, wasiamini kama kweli naye ni mwanafunzi.Matendo 9:26. Huwezi kuwalaumu wanafunzi kwa wasiwasi wao. Nisingemtaka mtu aliyeua wakristo mwezi uliopita akiongoza mafundisho ya Biblia! Wewe je?

Paulo alikuwa na tatizo. Alikosa kuaminiwa na wakristo wengine. Kwa hiyo Paulo alitoka na kumwendea yeyote ambaye angempa nafasi ya kushirikiana naye shauku yake mpya. Uamuzi wa Paulo kuungana haukubadili habari yake tuu, bali ulibadili historia. Unaona, Paulo alibakiza rafiki mmoja ili abadili njia ya hatima yake. Na huyo rafiki alikuwa na mtu anayeitwa Barnaba.  

Unaweza kuwa bado rafiki mmoja tuu kubadili habari yako.

Leo utasoma kuhusu wakati Barnaba alipohatarisha maisha yake kwa kumchukua Paulo kwa mitume, ambao walikuwa ni viongozi wa watu ambao Paulo amekuwa akijaribu kuwaua katika maisha yake ya awali. Nini kilitokea? Rafiki mpya wa Paulo Barnaba alihatarisha heshima yake kwa ajili ya Paulo. Na kwa sababu ya Barnaba, wanafunzi wengine walimpa nafasi Paulo. Yaliyoendelea ni hadithi. Unaweza kuwa bado rafiki mmoja tuu ili kubadili habari yako.

Bado rafiki mmoja tuu kufikia ndoa bora. Bado rafiki mmoja tuu ili ushinde ulevi. Bado kukiri mara moja tuu ili uwe vizuri. Bado mshauri mmoja tuu ili uelewe karama zako na kuwa kiongozi bora.

Jiulize:Natakiwa kufanya nini ili kuungana na watu sahihi? Je, kuna yeyote nahitaji kuachanishwa naye?

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Divine Direction

Kila siku tunafanya maamuzi ambayo yana unda hadithi ya maisha yetu. Maisha yako yangekuwaje kama ungekuwa bingwa wa kufanya maamuzi? Kwenye Mpango wa Biblia wa Mwongozo wa kimungu, mwandishi mzuri wa New York Times na Mchungaji Kiongozi, Craig Groeschel, anakutia moyo na kanuni saba kutoka kwenye kitabu chake cha Mwongozo wa Kimungu ili kukusaidia kupata busara ya Mungu kwa maamuzi yako kila siku. Gundua mwongozo wa kiroho unaohitaji ili kuishi hadithi ya maisha ya kumheshimu Mungu utakayopenda kuhadithia.

More

Kungependa kumshukuru mchungaji Craig Groeschel na LifeChurch.tv kwa kuweshesha mpango huu Kwa maelezo zaidi tafadhali temembelea: http://craiggroeschel.com/