Mwongozo wa KiMunguMfano
Go
Je, unahisi kuna kitu kipya kinatokea katika maisha yako? Unataka kitu cha tofauti? Hata kama huhisi sasa hivi, siku zote ni jambo jema kuuweka moyo wako tayari kwa mabadiliko kwa sababu ni lazima.
Tumeshazungumza kuhusu Kuanza, Kusimama, na Kukaa. Wakati mwingine uamuzi unaoweza kuufanya katika kumtafuta Mungu ni Kwenda.
Mara nyingi tumeitwa kusimama imara wakati wa msukusuko mkali, lakini mara nyingi tunahitaji kuchukua ujasiri. Unajisikia kutokutulia ulipo? Mungu anaweza kuwa amepanda shauku ndani yako ya kumtumikia kwa njia ya ajabu. Labada amekuvuvia kwa ajili ya kundi fulani la watu, wazo, tatizo, au mahali. Labda anakuita uondoke. Fuata njia ile uone inakupeleka wapi. Furahia safari. Njia bora ya hatua ya imani ni kuwa na mwanzo mzuri.
Kuna habari kuu katika agano la Kale kuhusu Abram na Sarai ( Baadaye wakaitwa Abrahamu na Sara) ambayo inaelezea "kwenda" vyema. Katika Mwanzo 12, Mungu alisema na Abram. Wakati huo, Abram alikuwa akiishi katika mji uitwao Harani lakini alikuwa anatoka mji wa Uru wa Wakaldayo. Huko mji wa nyumbani kwao Abram Uru, watu waliabudu mungu mwezi aliyeitwa Nana.
Kinachoonekana ni kwamba Mungu pekee wa kweli alijifunua
kwa Abram. Mungu akampa Abram amri rahisi na ya moja kwa moja: ondoka katika chochote ambacho umewahi kukijua. “Ondoka nchini mwako, watu wako na nyumba ya baba yako na nenda katika nchi nitakayokuonesha" Mwanzo 12:1, msisitizo wa kwangu
Ondoka na uende.
Kuchukua hatua kwenda kwenye hatima yako, unaweza kutoka katika mazingira ya usalama wako.
Kwenda mahali kwingine, lazima uondoke mahali ulipo. Lazima uache unavyojua, kilicho cha faraja, kitarajiwacho, na kilicho rahisi. Kuelekea hatima yako, lazima uondoke kwenye usalama wako.
Ni nani ajuaye wapi Mungu atapeleka habari zako kama utamruhusu? Siku moja, miaka ijayo, utaangalia nyuma katika maisha yako na kuona hadithi nzima. Itakuaje?, " Nilijisikia kama Mungu ananiita, lakini niliogopa, kwa hiyo sikufanya chochote." Au utakuwa na safari iliyojaa imani kusimulia? Tofauti ni kwamba utakwenda au hutaenda Mungu anapokuambia "nenda."
Ask: Je, Mungu ananiita niache nini? Ananiita niende wapi?
Kuhusu Mpango huu
Kila siku tunafanya maamuzi ambayo yana unda hadithi ya maisha yetu. Maisha yako yangekuwaje kama ungekuwa bingwa wa kufanya maamuzi? Kwenye Mpango wa Biblia wa Mwongozo wa kimungu, mwandishi mzuri wa New York Times na Mchungaji Kiongozi, Craig Groeschel, anakutia moyo na kanuni saba kutoka kwenye kitabu chake cha Mwongozo wa Kimungu ili kukusaidia kupata busara ya Mungu kwa maamuzi yako kila siku. Gundua mwongozo wa kiroho unaohitaji ili kuishi hadithi ya maisha ya kumheshimu Mungu utakayopenda kuhadithia.
More