Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

SIKU 25 YA 28

Baraka zinaweza kusambaa hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wampendao Mungu (m.4-5; “taa” hapa linamaanisha mtoto wa kutawala baada ya Abiya). Vivyo hivyo laana pia husambaa kwa wamchukiao Mungu. Hapa Abia ambaye ni kizazi kingine, anaanza kutawala Yuda. Lakini naye anaendeleza yaleyale waliyofanya baba na babu zake (m.3, Akaziendea dhambi zote za babaye, alizozifanya kabla yake). Tunawaachia watoto wetu urithi gani? Hata kama sisi tumeishi maisha maovu, tutubu na kuwaombea watoto wetu wasiingie kwenye laana ila wapate baraka.

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/