Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 16 YA 31

Luka anatusimulia tukio hili kama mfano hai wa maneno ya Yesu katika m.23 na 29-35 anapozungumza juu ya watu walivyompokea au kuchukizwa naye (kama una nafasi, soma mistari hiyo). Yule Farisayo Simoni hakumwalika Yesu kwa sababu alimpenda. Bali alitaka kumpeleleza. Na mara alichukizwa wakati Yesu alipokubali kutendewa jambo lisilo la kawaida na mwanamke mchafu (m.23 ambapo Yesu anasema, Heri mtu ye yote asiyechukizwa nami). Simoni ni kama mtoto akaaye sokoni akiitwa asiitike (m.31-32). Lakini Yesu hakutaka kumfukuza huyo mwanamke na dhambi zake, bali alifurahi mno kwa sababu amekuja kwake anayeweza kumwokoa. Alimwambia … Umesamehewa dhambi zako …. Imani yako imekuokoa, enenda zako kwa amani (m.48-50). Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye (Yn 3:17)! Huyo mama ni mtoto wa hekima, na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote (m.35) - Je, unampenda Yesu?

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...

More

http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha