Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 19 YA 31

Nakusihi usinitese (m.28). Hili ni ombi la watumishi wa Shetani kwa Yesu. Yesu ni Mkuu. Mbele yake Shetani hana nafasi kabisa! Kwa hiyo, ndugu Mkristo, huna sababu kuhofu nguvu za giza. Liitie jina la Yesu, ujikabidhi mikononi mwake kila siku! ‘Shimoni’ ni gereza la Mungu kwa malaika walioanguka pamoja na Shetani: Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu (2 Pet 2:4). Yesu atakapokuja kuudhihirisha utawala wake hapa duniani Shetani atafungwa shimoni kwa miaka 1000! Katika Ufu 20:1-3 imeelezwa wazi: Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache. Lo! itakuwa siku njema sana! Neno la kigriki lililotafsiriwa ‘jeshi’ ni ‘legeon’. Maana yake ni 6000.

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

http://www.somabiblia.or.tz