Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 17 YA 31

Katika miji na vijiji (m.1). Yesu hakuwa na ubaguzi. Hakutafuta kujijenga kwa watu wakubwa mjini ili apate sifa na mali ya dunia hii. Bali alitafuta sifa kwa Mungu, na kwa Mungu kila binadamu ana thamani kubwa akikaa kijijini au mjini, akiwa maskini au tajiri. Tufuate mfano wake tulio watumishi wa Bwana leo! Kuhusu mahitaji yake ya kila siku Mungu alimtunza kwa njia ya wanawake walioamini. Walikuwepo Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao (m.3). Yesu alitoa mfano uhusuo namna wanadamu wapokeavyo Neno la Mungu kwa njia tofauti. Tena alieleza maana ya mfano huo wa mbegu na mpanzi katika m.9-15. Je, wewe unafanana na nani?

Andiko

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

http://www.somabiblia.or.tz