Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 15 YA 31

Huenda watu walianza kupata mashaka juu ya Yohana Mbatizaji kutokana na kufungwa kwake gerezani - kama yeye mwenyewe alivyopata mashaka na kuwatuma wanafunzi wake wamwulize Yesu, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? (m.18-19). Mashaka ya Yohana Yesu aliyajibu kwa kuonyesha kwamba anayoyafanya ni yale yaliyotabiriwa na Maandiko kuhusu Masihi: Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema (m.22-23). Kuna maneno mengine ya Biblia yanayosema vivyo hivyo: Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa (Isa 26:19; ukipenda ling. Isa 35:5-6 na Lk 4:18-21). Mashaka ya watu Yesu aliyajibu kwa kuwaonyesha kwamba kazi ya Yohana ilikuwa ni kutimizwa kwa unabii: Huyo ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako mbele yako (m.27). Kwa namna ya Agano la Kale Yohana ni mkuu. Ila mambo anayoleta Yesu (Ufalme wa Mungu) ni makuu zaidi, tena sana. Kwa hiyo anaendelea na kusema katika m.28, Aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye (yaani, Yohana)!

siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...

More

http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha