Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 13 YA 31

Nawaambia, hata katika Israeli sijaona imani kubwa namna hii (m.9). Jeshi la Warumi lilikuwa na kituo kikubwa hapo Kapernaumu na huyu bwana alikuwa ni jemadari (‘akida’). Ni mwenye cheo kikubwa maana aliweza kuwajengea Wayahudi sinagogi. Ndiyo maana wanamwambia Yesu wakisema, Amestahili huyu umtendee neno hili; maana, analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi (m.4-5). Inaonekana kwamba alimwamini Mungu wa Wayahudi, maana kama m.5 unavyoonyesha, aliwapenda. Na imani yake ilikuwa ya kweli maana alimtambua Yesu na ukuu wake: sema neno tu (m.7). Ingawa ni mheshimwa sana katika mji huo alijiona si kitu mbele ya Yesu: sistahili. Omba uone zaidi ukuu wa Yesu!

Andiko

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...

More

http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha