Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano
Somo la leo lahusu kile tupandacho: Cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele (m.7-8). Imani yetu huonekana katika matendo yetu. Tukimpenda Yesu na Neno lake, upendo wetu uonekane kwa jinsi tunavyowatendea wanaoshughulikia kufundisha Neno la Mungu (m.6, Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote), na watu wote, hasa waaminio. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio (m.10). Tunaweza kulinganisha na 1 Yoh 4:20-21 inayotukumbusha kuwa mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake. Usimsahau mwinjilisti wako wala mchungaji wako walio na kazi mbili: kazi ya Mungu pamoja na kazi ya kawaida shambani! M.9 unasema: tusichoke! Labda hali yako si rahisi, lakini mtume Paulo anakukumbusha kwamba unalo tumaini.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/