Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano
Katika somo la leo mtume Paulo anatuita tujinyenyekeze. Watu ni wepesi kuhukumu; Kwa mfano katika Lk 9:51-56 tunaona wanafunzi wa Yesu wakitamani kuagiza moto uwaangamizi ambao hawakumkabirisha Yesu. Lakini Yesu anatuonya kuwa tusilaani kwa upesi. Hata sisi twaweza kujaribiwa. Basi mtu akighafilika akakosea, sisi tulio wa Roho tumrejeze upya kwa roho ya upole (m.1). Ujumbe wa m.2 ni kwamba leo ndugu yangu ana shida, kesho ingekuwa ni mimi. M.4-5 yasema kwamba tusiwe na haraka katika kuwapima ndugu zetu. Bali tuishughulikie na kuipima kazi yetu wenyewe, ili tusihukumiwe. 1 Kor 11:31-32 inaeleza vizuri, Kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa. Ila tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, isije ikatupasa adhabu pamoja na dunia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/