Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano
![Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F33134%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Leo tuchunguze maana ya yale ambayo "hayana sheria" (m.23b). Mambo ya Roho yaitwa tunda la Roho (m.22). Yaani, tunda hilo huzaliwa na Roho, siyo kazi yetu. Wajibu wetu ni kuongozwa na Roho: Tumia Neno la Mungu! Zingatia ilivyoandikwa katika m.24, Hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Maana yake ni kumpa Roho nafasi ya kuchunguza moyo wako ili umwungamie mabaya yako ambayo yameshafishwa msalabani. Rum 6:6-7 inaeleza kuwa mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. Kwa imani sisi tunashiriki katika kufa kwa Kristo, hivyo dhambi haziwezi kututawala. Katika Kristo hasira ya Mungu haipo kabisa juu yetu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F33134%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/