Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

SIKU 17 YA 30

Mkazo wa somo la leo ni kutukumbusha kwamba watendao dhambi hawatarithi ufalme wa Mungu (m.21b). Dhambi zinazotajwa ni pamoja na uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo (m.19-20). Kwa hiyo hatuwezi kutoa udhuru tukisema, “Tumeshindwa kufanya mema”, au, “Tusiwe watumwa chini ya sheria”. Kumfuata Roho, maana yake ni kupinga dhambi. Twaona kuna dhambi za aina mbalimbali katika m.19-21, ‘dhambi kubwa’ na ‘dhambi ndogo’. Lakini zote huwaelekeza watendao Jehanum. Kwa hiyo tuzipinge zozote wala kuzificha, bali tuziungame. Omba Zab 139:23-24 ukisema, Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu; Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele.

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/