Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

SIKU 16 YA 30

Mkazo wa somo unasomeka katika m.13. Tunasoma, Ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. Kuna makosa makuu mawili miongoni mwa Wakristo: 1. Kujaribu kujiokoa kwa njia ya sheria. 2. Kuendelea katika dhambi tukijitetea kuwa tumeokolewa kwa neema, basi tusijali kutii amri. Njia zote mbili hukuelekeza Jehanum! Kuishi katika mojawapo la makosa ya hapo juu huleta hali ya m.15 usemeao, Mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana. M.16-18 inahusu Roho kushindana na mwili: Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Hatuwezi kufanya mema tu, lakini tukienenda kwa Roho, tunaishi katika hali ya toba na ondoleo la dhambi. Katika 1 Yoh 1:5-10 Yohana anasema, Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake. Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/