Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

SIKU 21 YA 30

Somo la leo ni hitimisho la waraka huu kwa Wagalatia. Hapo mtume Paulo anarudia mambo fulani yaliyo na maana (m.12-17): 1. Hata wanaojivunia sheria hawaishiki, ingawa waliwalazimisha Wagalatia kuishika. Wataka tu wasifiwe kwa sababu ya tendo la kimwili la Wagalatia. 2. Kinyume cha hayo mkazo wa mtume Paulo ni katika imani. Fahari yake ni katika Yesu kumfia msalabani na matokeo yake: Sisi tumeona na kushuhudia ya kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu (m.14). Ujumbe ufuatao ni kwa hao tu wanaomwamini Kristo.Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake (m.16). Tuenende katika imani tukimwamini aliyetufia.

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/