Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano
Huu ni ushahidi wa Daudi. Tegemeo lake na imani yake ilikuwa katika Bwana. Je, ni ushahidi wako pia? Kuna sehemu mbili: 1. Kujisikia salama kabisa kwa sababu ya kuwa chini ya uchungaji wa Bwana (m.1-4). 2. Kumfurahia Bwana kwa sababu ya ukarimu na wema wake na kuimba hivi kama Daudi, Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele (m.5-6). Daudi alijua kwamba wanyama wa kufugwa ni dhaifu. Bila mchungaji hupotea na kufa. Ndivyo tulivyo sisi wanadamu kiroho. Ni wenye dhambi. Ni wepesi kunaswa na Shetani. Ila Yesu ndiye mchungaji mwema! Anatupenda! Ana uwezo wa kutulinda!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/