Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano
Baadhi ya wazee walikumbuka hekalu la Sulemani. Labda walisema, “Hekalu jipya halipendezi kama la kwanza.” Ili wajenzi wasitahayarike, Hagai anawatia moyo, “Hakika Mungu ni mwaminifu. Ni pamoja nanyi kama alipowatoa wana wa Israeli Misri.” Kupitia hekalu, Mungu atatikisa mbingu na nchi na mataifa yote ili walete dhahabu na fedha na kupamba nyumba yake, na itapewa utukufu na heshima kuliko wazee hao walivyohisi. Hali ngumu ya wajenzi si kitu ikilinganishwa na mafanikio yajayo, maana katika Ufu 21:22-27 tunasoma, Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake. ... Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake. Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku. Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake. Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/