Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano
Tunakumbushwa maonyo ya Mitume kwamba walimu wa uongo watasababisha matatizo katika kanisa. Tutaepukaje ushawishi wao mbaya? Yuda alianza na kutusihi tuishindanie imani; sasa anasema tujijenge juu ya hiyo imani (m.20, Wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu). Angalia jinsi Mungu mwenyewe ni mjenzi mkuu: Roho Mtakatifu anatusaidia kuomba, upendo wa Mungu unatulinda, na rehema ya Yesu inatupatia uzima wa milele (m.21, Jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele). Na siku moja atatuleta mbele yake mbinguni kwa ushindi mkuu. Basi, tumshangilie pamoja na Yuda, tukisema, Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu; Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina (m.24-25).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/