Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Majira mapya yenye heri yanatangazwa. Taabu zinaelekea mwisho. Hali ya amani inakuja. Inakujaje? Ukuhani na utawala wa kifalme vinawekwa pamoja. Akitawazwa Kuhani mkuu, ni tendo la ishara ya utawala mkamilifu. Mmoja aitwaye Chipukizi atakuja kujenga hekalu la Mungu kwa upya. Utukufu hautakuwepo katika jengo, bali katika mtawala huyu wa kimasihi. Linganisha na maneno yafuatayo: Siku hiyo chipukizi la Bwana litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka (Isa 4:2) Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani (Isa 9:6). Tutashiriki katika hayo yote ikiwa tuna utii kwa Mungu (m.15, Haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti ya Bwana, Mungu wenu). Anayetimiza yote ni Kristo Yesu. Hivyo Paulo anaweza kuwaandikia Wakristo wa Efeso: Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana (Efe 2:20-21).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/