Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Uelewa wa kawaida kuhusu kufunga ni kuachana na furaha. Watu wakifunga, huvaa huzuni na uchungu. Hapa kuna tangazo la kubadilisha siku za mfungo kuwa sikukuu za kuchangamkia. Kwa nini? Mungu yu pamoja nao! (m.23). Yeye akiambatana na watu wake, Israeli itakuwa kimbilio na baraka kwa wote. Kuu katika yote ni kupenda na kuziishi kweli na amani. Yerusalemu utakuwa kimbilio, na mtu wa Mungu atakimbiliwa, kwani wema wa Mungu utaonekana hapo. Kwa uelewa zaidi, tafakari maneno yafuatayo, Watakujilia, nao watakuwa wako; watakufuata; watakuja katika minyororo; wataanguka chini mbele yako, watakuomba, wakisema, Hakika Mungu yu ndani yako; wala hapana mwingine, hapana Mungu tena (Isa 45:14). Wote wakihutubu, kisha akaingia mtu asiyeamini, au mjinga, abainishwa na wote, ahukumiwa na wote; siri za moyo wake huwa wazi; na hivyo atamwabudu Mungu, akianguka kifudifudi, na kukiri ya kuwa Mungu yu kati yenu bila shaka (1 Kor 14:24-25).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/