Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi (m.5). Maneno haya yanaonyesha kwamba habari ya Injili ni habari ya kihistoria. Ni mambo yaliyotokea kweli, mahali fulani, wakati fulani! ”Uvumba” (m.8-9) ni sawa na ubani. Sheria kuhusu kufukiza uvumba inasema, Fanya madhabahu ya kufukizia uvumba; utaifanyiza kwa mti wa mshita. ... Nawe utaitia mbele ya lile pazia lililo karibu na sanduku la ushuhuda mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, hapo nitakapokutana nawe. Na Haruni atafukiza uvumba wa manukato juu yake; kila siku asubuhi atakapozitengeneza zile taa, ataufukiza (Kut 30:1 na 6-7). Wana wote wa ukoo wa Haruni walikuwa makuhani. Wakati wa mfalme Daudi waligawanyika katika zamu 24. Zamu mojawapo ni ya Abiya (m.5; zamu hii imetajwa pia katika 1 Nya 24:10). Wajibu wa yule mtoto utakuwa kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa (m.17).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/