Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

SIKU 16 YA 31

Hali mpya ya amani na haki haitokani na ubora wa watu, bali Mungu ameamua kutazama watu wake kwa neema. Katika m.10-12 imeelezwa jinsi Israeli ilivyokuwa laana katika mataifa Mungu alipowaacha, Kabla ya siku zile hapakuwa na ijara kwa mwanadamu, wala hapakuwa na ijara kwa mnyama; wala hapakuwa na amani kwake yeye aliyetoka, wala kwake yeye aliyeingia, kwa sababu ya adui; nami nalimwacha kila mtu kugombana na jirani yake. Lakini sasa sitakuwa kwa mabaki ya watu hawa kama nilivyokuwa siku zile za kwanza, asema Bwana wa majeshi. Kwa maana itakuwako mbegu ya amani; mzabibu utatoa matunda yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na hizo mbingu zitatoa umande wake; nami nitawarithisha mabaki ya watu hawa vitu hivi vyote. Ndivyo Israeli itakavyokuwa baraka awaokoapo, Kama vile mlivyokuwa laana katika mataifa, Ee nyumba ya Yuda, na nyumba ya Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka; msiogope, lakini mikono yenu na iwe hodari (m.13). Lipi lifanyike sasa? Mara mbili Mungu anarudia wito: Mikono yenu na iwe hodari (m.9 na 13). Watu wasiogope, bali wawe hodari katika neema ya Mungu. Hiyo ndiyo inayotutia moyo, na kutufundisha na kutuwezesha kusema kweli na jirani yetu, kutowaza mabaya juu yake n.k.

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/