Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Siyo rahisi kuelewa maana yote ya maono kuhusu magari ya vita manne. Lakini bila shaka yanaonesha ukuu wa Mungu na mamlaka yake juu ya uumbaji wote. “Pepo nne za mbinguni” zimeelezwa katika Zab 104:4, Huwafanya malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa moto wa miali; na katika Isa 66:15, Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. Magari yanakwenda kasi kuelekea sehemu nne za dunia ili kueneza utawala wa Mungu popote na kuimarisha ufalme wake. Mungu ni BWANA, na ukuu wake haushindanishwi na chochote wala yeyote. Mtu wa Mungu, unashauriwa kuishi kwa kutegemea uwepo wa Mungu, ili upate utulivu utoshao: Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako, Usiondoke mara mahali pako ulipo; Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa (Mhu 10:4).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/