Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

SIKU 10 YA 31

Vipi na uovu uliotapakaa katika jamii? Maono ya efa (= kikapu) na mwanamke yaonyesha jinsi nchi ya Israeli hatimaye itakuwa huru mbali na ushawishi wa uovu. Shinari ni sawa na Babeli, mahali pa kuabudu sanamu au miungu. Licha ya ibada hizi mara nyingi kuunganishwa na uasherati, zilihesabiwa kuwa uzinzi wa kiroho. Katika Ufu 14:8 imeandikwa, Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake. Mfano huohuo wa uzinzi umetumika katika Ufu 17:5, Katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI. Roho wa Mungu ataangamiza hali hiyo kati ya watu wake. Hatimaye Mungu atatawala uumbaji na taifa lake. Tumwombe atuwezeshe kuutambua uovu huo tusinaswe nao.

Andiko

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/