Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Wayahudi walikuwa wamejiwekea siku za kufunga ili kuomboleza matukio mabaya katika historia ya taifa lao miaka 70 iliyopita. Linganisha na 8:18-19 ambapoBwana wa majeshi asema hivi, Saumu ya mwezi wa nne, na saumu ya mwezi wa tano, na saumu ya mwezi wa saba, na saumu ya mwezi wa kumi, zitakuwa furaha na shangwe, na sikukuu za kuchangamkia, kwa nyumba ya Yuda; basi zipendeni kweli na amani. Sasa, hekalu jipya likiendelea kujengeka, je, bado waadhimishe siku hizo za kufunga? Jibu ni kwamba kufunga na maadili pasipo kuliishi Neno la Mungu ni bure. Wasirudie dhambi za mababu zao, bali waonyeshe utii wao kwa Mungu wakitenda haki na rehema: Fanyeni hukumu za kweli, kila mtu na amwonee ndugu yake rehema na huruma ... (m.9-10). Jambo hili linatiwa mkazo vile vile katika Isa 58:4-7, Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/