Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Wayahudi walioishi wakati wa Zekaria wanaitwa kujifunza ujumbe wa matokeo ya kihistoria, mababu zao walipobeza Neno la Mungu kupitia manabii wake. Kila tulicho nacho mwilini ni kwa kumtumikia Mungu, lakini hawakutumia masikio yao kusikiliza, mabega yao hawakuyaelekeza kwa Mungu, wakaziba viungo vya kusikilizia kwa Mungu. Matokeo yake, wakaifanya mioyo yao kukakamaa, maisha yao yakapishana na Mungu, wakamghadhabisha aliyewaumba na kuwakomboa. Ukaidi ni hasara. Bila sauti ya Mungu unaachwa mkiwa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/