Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano
Esauakaenda mpaka nchi iliyo mbali na Yakobo nduguye. Maana mali yao yalikuwa mengi wasiweze kukaa pamoja ... Esau akakaa katika mlima Seiri(m.6-8). Sura hii inatoa maelezo mengi kuhusu Esau na watoto wake. Ila baadaye hatupati tena habari yake. La muhimu ni kwamba sababu yao ya kuachana si chuki, bali ni nafasi kuwa ndogo, wasiweze kukaa pamoja. Na Esau alikubali kwamba Yakobo ndiye aliyeahidiwa nchi ya Kanaani! Akahamia mahali pengine. Uhusiano huu mzuri ulitakiwa kuendelea (ukiwa na nafasi, jisomee pia Kum 2:1-8).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/